Tuesday, August 19, 2008

RAFIKI BORA KIBIBLIA




Kuwa na marafiki ni jambo jema na lakupendeza! lakini wakati mwingine marafiki wengine watakutumbukiza katika shimo na utagundua tayari umeshachelewa! Ni vyema ukaangalia katika marafiki ulionao wanakufaa wangapi! ambao hawana faida kwako waepuke, ikibidi achana nao.
Mfano wa marafiki wazuri katika biblia:-
RUTHU (Ruth 1:1-22)- Atakaye kuwa nawe hata katika nyakati ngumu. Naomi alimwambia Ruthu arudi lakini yeye alisema “Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe, maana uendako nitakwenda, ukaapo nitakaa” J
JONATHAN (1 Samweli 20:1-42) - Yuko tayari kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya rafiki yake. Jonathan alimsaidia Daudi, maisha yake yalikua hatarini baada ya mfalme Sauli kutaka kumuua. Alimwambia “lolote utakalonifanye, Nitafanya kwa ajili yako”
PAULO (1 Korintho 4:14-6:20) - ‘Anayesaidia rafiki zake wakue katika kumjua Mungu, kuwatia moyo na kuonya.’
YESU - Rafiki wa kweli!! mwenye upendo wa dhati. Kuwa rafiki mzuri tujiunganishe kwa Yesu atatufundisha jinsi ya kuwa rafiki mwema (Wakolosai 3:12-17)
Sasa, Tuone mfano wa marafiki wabaya:-
Akida wa farao (Mwanzo 40:1-23) - Yusufu alimtafsiria ndoto na akida alimuhaidi akitoka jela Yusufu ataachiliwa. Lakini alipoondoka pale, hakumkumbuka Yusufu.
Ahithofeli ( 2 Samweli 15:12-17:23) - Mshauri wa Daudi mnafiki, Daudi alimuamini sana lakini alikuwa akivujisha siri za mfalme kwa maadui.
Yuda Iskarioti (Mathayo 26:15-17, 25; Luka 22:47-48)- alijidai kuwa rafiki lakini alikuwepo nao kwa maslahi yake binafsi. Msaliti
Hii ni baadhi ya mifano bila shaka nanyi mtakuwa na mingine ambayo inaonesha ni aina gani ya marafiki wabaya na marafiki wazuri. Mungu awatunzeni!

No comments: